Padri Evarist Mushi |
Padre wa Kanisa la Katoliki la parokia ya Minara Miwili lililopo mji mkongwe, Zanzibar, Padri Evarist Mushi amepigwa risasi ya utosini na kufariki papo hapo na watu wasiojulikana.Padri huyo alikuwa akielekea kuendesha misa ya saa 3 asubuhi hii (kwa saa zaTz) kwenye kanisa la Mt. Theresia na akiwa eneo la Mtoni ndipo alisimamishwa na watu wawili waliokuwa wamepakizana katika katika pikipiki aina ya Vespa wakampiga risasi.
Mashuhuda wanasema, baada ya tukio hilo gari hilo liliacha njia na kugonga nyumba moja iliyokuwa karibu na kanisa hilo.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali kuu ya Zanzibar iliyopo Mnazi Mmoja. Sababu za kupigwa risasi kwa Pari huyo bado hazijafamika.
Matokeo haya ya kihalifu yanayozidi kuendelea kutokea Zanzibar ni jambo la kusikitisha sana.
Tutaendelea kuwajuza kwa kila taarifa itayopatikana.
No comments:
Post a Comment