Tuesday, May 28, 2013

Kilichomuua Ngwear hiki hapa


Albert Mangwea aka Ngweair of Cowwizy
Taarifa ambazo Lenzi ya Michezo imezipata kutoka South Africa kwa Hussein Original ambaye yupo Pretoria, amesema Ngwear amefariki leo asubuhi kwenye ghetto ambalo alikuwepo pia msanii M to The P ambaye yeye amelazwa hospitali akiwa mahututi. 

"Tulivyokwenda kuwagongea asubuhi tuliwakuta Ngwear amefariki na M To The P akiwa amepoteza Fahamu Kabisa"

Baada ya kuwapeleka hospitali daktari alithibitisha amekufa na ameshatoa taarifa kwa watu wa karibu wa Ngwear huko Afrika ya Kusini.

Ngwea akiwa na msanii M to the P walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezimia kwenye chumba wote wawili baada ya kuzidisha (overdose) madawa ya kulevya .


Hata hivyo mama yake Ngwear ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afrika ya Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.


Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwear ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili kesho Morogoro.

No comments:

Post a Comment