Sunday, June 16, 2013

Houston wamfanyia Marehemu Jerome Mpefo Harambee ya kishindo

Jioni ya leo katika ukumbi wa Lutheran Memorial, Houston Jumuiya ya Watanzania imefanya harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Jerome Mpefo. Harambee hiyo iliyohudhuriwa na Wanajumuiya wengi iliendeshwa vyema kwa ushirikiano wa kaka Domino na James Shemdoe wakisindikizwa na Dj Jimmy. Pesa taslimu zilichangwa pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa na wanajumuiya kunadiwa ilikuwa ya kufana na ilipitisha lengo lililowekwa la kukusanya $17,000 .Hadi mwisho wa Harambee jumla ya $33,055 zilipatikana na hivyo kuvuka lengo kwa 194%. Mungu awabariki wote waliotoa kwa moyo. Pata baadhi ya picha za matukio katika shughuli hiyo.

Marehemu Jerome

No comments:

Post a Comment