Thursday, August 1, 2013

NBA Star STEPHEN CURRY yuko Dar kuendesha kliniki ya kikapu Don Bosco

Wardell Stephen "Steph" Curry II

Mkali wa Point tatu ligi ya marekani (NBA) Msimu wa 2012-2013, STEPHEN CURRY anatarajia kuendesha clinic maalum jijini Dar katika viwanja vya DON BOSCO OYSTERBAY. Clinic hiyo maalum itafanyika kesho, 1 August kuanzia mida ya saa tatu asubuhi hadi saa tisa mchana.
Akiripoti kupitia account yake ya Facebook, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF) PHARES MAGESA alisema mkali huyo kutoka timu kali Inayoshiriki Ligi kuu ya kikapu Marekani GOLDEN STATE WARRIORS(GSW), Amekuja nchini Tanzania kupitia mpango wa Malaria wa UN FOUNDATION.

Ukiachana na shughuli hizo za Kijamii za vita Dhidi ya Malaria,CURRY atatumia muda huo kufanya Clinic fupi itakayoshirikisha vijana 100 wakitazania wenye umri kati ya miaka 14-18.Vijana hao ni pamoja na watakaotoka katika mashule na vilabu mbali mbali vya kikapu jijini Dar es salaam. Akitaja mgawanyiko wa vijana watakaoshiriki ni pamoja na MABIBO(5), MONTFORT(5), POLIS(5), STREET WORRIES(5), CHUI(5), CHANG'OMBE(6),OUTSIDERS(5),VIJANA(7), AIRWINGS(5),TUSIIME(8),LORD BADEN(5),DON BOSCO UPANGA(7), JKT MGULANI(5), HEROIS(5), ALI HASSANI MWINYI(5), DON BOSCO OYSTERBAY (11). 

Pia clinic hiyo itahudhuliwa na Makocha wa Wazawa akiwemo SAJDA AHMED NA AGNELA SEMWAIKO(SAVIO), JEVERINO PEMBE(MABIBO),KABLOLA SHOMARI(VIJANA), MOHAMMED MBWANA(CHANG'OMBE),WILLIAM MZIRAY (OILERS), na ROBERT MANYERERE (UDSM OUTSIDERS). 

Wasimamizi wa shughuli nzima uwanjani watakuwa ni BAHATI MGUNDA(VIJANA) NA EVARIST MAPUNDA(PAZI). Wadau wote wa Basketball wanakaribishwa kuhudhulia clinic hii ili kuweza kujifunza kitu kutoka kwa Stephen Curry.

No comments:

Post a Comment