Sunday, December 8, 2013

Makamba atembelea darasa la Kiswahili DMV

 Naibu Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknologia, Mhe. January Makamba akiongozana na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga siku ya Jumamosi Dec 7, 2013 College Park Maryland, siku alipotembelea darasa la Kiswahili DMV.
 Mhe. January Makamba akisalimiana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania mara tu alipoingia kwenye darasa hilo Jumamosi Dec 7, 2013 College Park, Maryalnd.
 Mhe. January Makamba akipata historia fupi ya darasa hilo kutoka kwa rais wa Jumuiya Iddi Sandaly (wapili toka kushoto) siku ya Jumamosi Dec 7, 2013 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia alipotembelea darasa hilo College Park Maryland.
 Mhe. January Makamba akisalimiana na wazazi wa watoto wa darasa la kiswahili DMV.
 Mhe. January Makamba akipata maelezo kuhusiana na watoto wa darasa la kiswahili DMV kutoka kwa katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Amos Cherehani (kulia koti jeusi).
 Watoto wa darasa la kiswahili DMV wakitoa salamu kwa mhe. January Makamba (hayupo pichani)
 Mhe. January Makamba pamoja na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Rais wa Jumuiya Iddi Sandaly na mwalimu mkuu wa darasa la kiswahili wakiwa wamesimama wakati watoto wa darasa la kiswahili waliopkuwa wakiimba wimbo wa taifa.
 Watoto wa darasa la kiswahili wakimwimbia mgeni wao Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba wimbo wa Taifa.
 Juu na chini baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, watoto wa darasa la kiswahili na wazazi wakimsikizliza Mhe. January Makamba (hayupo picha) alipokua akiwathimilia hadithi watoto wa darasa la kiswahili DMV.

<

No comments:

Post a Comment