Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston, Texas jioni ya leo imefanya mdahalo wa wagombea nyadhifa za Uenyekiti na Ukatibu mkuu wa jumuiya katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.Nafasi ya mwenyekiti inagombewa na Bw.Issa Kingu, Bw.Erasto Mvungi, Bi.Nuru Mazora na Bw.Isaiah Mgendi.Wakati nafasi ya Ukatibu inagombewa na katibu anayemaliza muda wake Bi.Leyla Kikuzi na Bw.Alfred Nkunga.
Mdahalo huo ulioandaliwa na Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Bw.Steve Maonyesho na kuendeshwa na Bw.James Shemdoe (Moderator) ulihudhuriwa na idadi ya kuridhisha ya Watanzania waishio katika jiji hilo la Houston na kurushwa live kupitia mtandao kwa wale ambao hawakuweza kuhudhuria. Zifuatazo ni picha za tukio hilo.
Wagombea nafasi ya Mwenyekiti toka kushoto Bw.Mgendi , Bw.Mvungi na Bw.Kingu |
Moderator wa Mdahalo Bw.Shemdoe |
Bw.Nkunga akiuza sera |
Wagombea |
Shughuli inaendelea |
Sehemu ya wanajumuiya wakisikiliza sera za Wagombea |
Bi.Leyla akimwaga sera |
Cameraman Bw.Fue |
Dk.Tenende akifuatilia mdahalo kwa makini |
Maswali yakiendelea kuulizwa |
Wagombea |
Bw.Mgendi akimwaga sera |
Wenye Jumuiya yao |
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Bw.Maonyesho |
Mwenyekiti anayemaliza muda wake Bw.Novatus Simba akichangia |
Dk.Tenende na Bw.Andrew Sanga |
No comments:
Post a Comment