Sunday, February 9, 2014

TASWIRA YA SHEREHE ZA KUZALIWA CCM TAWI LA NEW YORK PITIA CHINI

Tawi la CCM New York walivyoshereheka miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho, Kulikuwa na  hotuba ya viongozi wa tawi na mgeni rasmi kutoka Tanzania UN Mission Mama Maura Mwingira. Historia ya chama  iliyosomwa na mwenyekiti wa tawi bwana Maftah na mambo mengi kama kula chakula  kucheza ngoma na muziki kutoka kwa Dj Paul Masoud wa Boston.
Mgeni rasmi  akiingia ukumbini hapa akisindikizwa na viongozi wa tawi la CCM New York. 
Viongozi wakijiweka sawa kwenye meza kuu
 Meza kuu ikiwa na viongozi wa tawi pamoja na mgeni rasmi katika sherehe hiyo mama Maura Mwingira katika katika
 Katibu wa tawi la CCM bwana Shaban Mseba akiongea kabla ya kamkaribisha mgeni rasmi kuongea 
Mama Maura Mwingira mgeni rasmi katika sherehe hiyo akiongoa, Mama Maura W. Mwingira, ni Minister Plenipotentiary Mission of the United Republic of Tanzania to the United Nations
Bwana Maftah mwenyekiti wa tawi la CCM New York akisoma hotuba fupi ya chama hicho.
Bwana Isaack Kibodya akisoma historia ya CCM na Tanzania kwa ujumla.
Mchereheshaji wa cherehe hiyo Gaston akitoa ratiba ya sherehe mzima ukumbini hapo
Mgeni rasmi akichukua chakula, sherehe hii ilisimamiwa na vijana wa New York wanaojulikana kwa jina la Zima Taah. Zima Taah ni kikundi cha vijana wa New York kinachoongozwa na viongozi wa muda katibu na mwenyekiti wake Bahia na Gaston. Hongera sana wanazima taah kwa kazi mzuri ya kufanikisha shughuli hii, kwa picha zaidi jitiririshe chini.

No comments:

Post a Comment