Monday, March 24, 2014

Balozi Mulamula kusimika Uongozi mpya wa Jumuiya ya Watanzania Houston

Balozi Liberata Mulamula
Tunapenda kuwatangazia kwamba siku ya Jumamosi tarehe 29 machi 2014, jumuiya yetu ya Watanzania Houston itafanya sherehe ya kusimika viongozi wapya wa jumuiya. Muda ni kuanzia saa mbili kamili jioni(8pm) katika anuani ifuatayo:

Turquoise Center, 9301 West Bellfort Ave. Houston TX 77031.

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania hapa US na Mexico, Mh.Liberata Mulamula ndiye atakaekuwa mgeni rasmi wa tukio hili la kihistoria katika jumuiya yetu ya Houston. Wote mnakaribishwa ili tusherekee na tuweke historia hii kwa pamoja.

Pia siku hii ya tarehe 29 machi 2014, afisa wa uhamiaji kutoka Ubalozi wa Tanzania,Washington DC atakuwepo ili kutoa huduma ya pasi za kusafiria(passport) kwa Watanzania wanaoishi hapa Houston na vitongoji vyake, pamoja na miji jirani. Huduma ya pasi(passport) itatolewa kuanzia saa tatu asubuhi(9am) mpaka saa kumi na moja jioni(5pm) katika anuani ifuatayo:

  • 9950 westpark drive. Houston TX 77063. Suite # 124. 
  • Simu(phone): 832-804-8999


Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Stephen Maonyesho 713 834 4839 au 
Novatus Simba 832 208 8344

Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki wenu,karibuni sana.
Asanteni,
Novastus Simba,Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania Houston

No comments:

Post a Comment