Kijana Prince mzaliwa wa Dar es Salaam ameonyesha kiwango kikubwa cha soka katika umri mdogo wa miaka 9 akiwa anaishi na wazazi wake nchi ya Norway. Kijana Prince anaonekana kufuata nyayo za baba yake Allan Mlagulwa ambaye enzi zake alikuwa middle hatari katika shule ya Buhangija, Mihogoni, Tambaza na Mzumbe na vile vile timu za mtaani kama Abajalo, Sinza Starz na Mji Mpwapwa kabla hajatundika daluga nakuamua kuwa meneja wa kijana wake.
Pata picha za Prince akiwa kwenye mechi ya watoto iliyofanyika hivi karibuni katika jiji la Oslo ambapo timu yake ilishinda bao 10-3 yeye peke yake akitupia bao 7.
|
Prince kushoto akimtia njaa beki wa timu pinzani |
|
Kijana akionyesha skills ambazo wakinamama wakizungu wanatamani angekuwa ni mtoto wao |
|
Mawaidha kutoka kwa kocha |
No comments:
Post a Comment