Ndugu Wanajumuiya:
Kwa masikitiko makubwa, tunatangaza kifo cha mwanajumuiya mwenzetu, Ndugu Peter Wilson Chapanga.
Marehemu Peter Wilson Chapanga, 36, amekutwa na mauti ghafla leo saa 11:30 jioni, Jumatano Juni 18, 2014, kwa mshtuko wa moyo (massive heart attack) huko St. Joseph’s Medical Center.
Marehemu aliyekuwa anaishi Pearland, TX, ameacha mke, Bibi Lakenya Perry. Pia, marehemu ni ndugu ya mmoja ya mwanajumuiya, Bi. Rona Lyimo.
Wafiwa wanapatikana katika nambari zifuatazo za simu:
Bibi Lakenya Perry Wilson: 713 557 9843
Bi. Rona Lyimo: 832 335 2009
Tutaendelea kuwapa taarifa kuhusu ulipo msiba na mipango mingine kadiri tunavyozipokea.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Idara ya Mawasiliano/ Uhusiano
Tanzania Houston Community
No comments:
Post a Comment