Thursday, September 18, 2014

Taarifa Rasmi ya Maendeleo ya Misiba Houston kutoka kwa Uongozi wa THC

Ndugu Wanajumuiya:

Poleni sana kwa misiba iliyotupata. Tuendelee kuwatembelea na kuwafariji wafiwa katika kipindi hiki kigumu.

Ifuatayo ni ratiba fupi ya awali ya shughuli za maombolezo ya pamoja na ndugu zetu wafiwa. Tunaomba mtenge muda na kujitahidi kufika kwa wingi ili kuwafariji wenzetu.

1. Leo Alhamisi Septemba 18, 2014 kutakuwa na kikao cha maandalizi ya shughuli za kumsindikiza ndugu yetu Marehemu Method C. Mengi:


  • Wapi? 21911 Sunvolt Ct.,Richmond, TX 77407 (nyumbani kwa Bw. Makangula)
  • Muda? Saa 2 jioni (8pm)
  • Agenda? Bajeti ya Msiba, Mipango ya Harambee na Kitabu cha rambirambi 

2. Jumamosi Septemba 20, 2014 kutakuwa Harambee ya Msiba wa Marehemu Method C. Mengi:


  • Wapi? Taarifa itatolewa leo jioni au mara itakapothibitishwa
  • Muda? 10 alasiri – 1 jioni (4pm - 7pm).


3. Jumapili Septemba 21, 2014 kutakuwa na ibada ya kumwombea Marehemu Hawa Kiwanuka, mama mzazi wa ndugu yetu Bi Hidaya Kiwanuka:


  • Wapi? Taarifa itatolewa leo jioni au mara itakapothibitishwa
  • Muda? Taarifa itatolewa na ukumbi


Tutazidi kupeana taarifa kadiri zinavyojiri. Tafadhali washirikishe taarifa hizi ndugu, jamaa na marafiki.

Siku njema.


Imetolewa kwa niaba ya wafiwa.


No comments:

Post a Comment