Monday, October 6, 2014

DICOTA 2014 Convention Gala Dinner yafana

 Msanii wa vichekesho Masanja Mkandamizaji akisalimia wadau kwa kuwavunja mbavu kwenye DICOTA 2014 Gala Dinner iliyofanyika Ijumaa usiku Oct 3, 2014 katika Hotel ya Millennium Durham, North Carolina nchini Marekani kwenye Gala Dinner kulitolewa vyeti kwa wadhamini wa ndani na nje ya Marekani waliowezesha DICOTA 2014 Convention kuwa ya mafanikio.Waliowezesha DICOTA 2014 Convention kupata mafanikio kuanzia uongozi wa juu wa DICOTA mpaka kamati ya maandalizi wakaazi wa North Carolina wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi Bw. Alphayo Kidata, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mkuu wa kitengo cha Disapora Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Rosemery Jairo
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea machche kuwashukuru Viongozi wa DICOTA na kamati nzima ya maandalizi kwa kuwezesha kufanikisha DICOTA 2014 Convention na kuwaasa daima wawe na malengo ya kuangalia mbele na kuweza kumkomboa mwanadiaspora katika katika nyanja mbalimbali za maendeleo na hatimae mwanadiaspota atumie  ujuzi na ufanisi wa maendeleo hayo kusaidia nyumbani.


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea machche na kutoa shukurani zake kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa kukubali kuja na kuendelea kuwa na Imani na DICOTA pia alipata nafasi ya kuwashukuru wadhamini toka Tanzania bila kumsahau mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rosemery Jairo.Katika Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakibadilishana mawili matatu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kwenye DICOTA 2014 Convention Gala Dinner.

Mkuu wa kitengo cha Disapora Bi. Rosemery Jairo akiwa katika picha na Dr. Samakula.

 
Juu na chini ni Fashion show kwenye gaka dinner ya Dicota 2014 Convention
 Juu na chini fashion show ya Kwetu fashions by Missy TemekeJuu na chini ni utoaji vyeti kwa wadhamini wa DICOTA 2014 Convention

Juu na chini ni uotoaji vyeti na tuzo kwa washindi wa DICOTA 2014 Convention kwa wadau wa diaspora katika nyanja tofauti.
 Washindi wa tuzo katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

No comments:

Post a Comment