Monday, November 10, 2014

Maonyesho ya Career Africa yafana New York

Sophia Yona mwanadiaspora wa New York akiuliza jambo kwa mwakilishi wa Exim Bank Bwn. Dinesh Arora kwenye Career Africa iliyofanyika jiji lisilo lala New York City ndani ya hotel ya Hilton iliyopo mtaa wa 1335 avenue of americas, New York New York 10019 na wanaDiaspora takribani 400 walijitokeza kwenye Careear Africa hiyo iliyokua imeandaliwa na baadhi ya wana Diaspora wa New York na New Jersey kwa kushirikiana na makampuni makubwa yanayofanya shughuli zake Afrika yaliyofanya kongamano hilo kwa ajili ya kuwatafuta wanaDiaspora wa Marekani wanaopendelea kufanyakakazi kwenye makampuni yao. Makampuni yaliyoleta wawakilishi  ni AXA insurance, Exim bank, national Microfinance Bank (NMB). OCP group, PZ Cussons, Safaricom na Tollow Oil.
Bi. Rokyaya Mane (kulia) mwakilishi wa National Micfofinance Bank (NMB) akitoa maelezo kwa wanaDiaspora waliohudhuria kongamano hilo lililoandaliwa maalum kutafuta wanaDiaspora wanaopendelea kuajiliwa na makampuni hayo Kongamano la Career Africa lililofanyika kuanzia Ijumaa Novemba 7-9, 2014 jijini New York City.
Bwn. Alaoui Banachem (kulia0 mwakilishi kutoka OCP Group akitoa maelezo kwa mwanaDiaspora huku akijaribu kuinadi kampuni yake kwa madau.
WanaDiaspora waliohudhuria kongamano la Career Africa wakibadilishana mawasiliano.
Kushoto ni Bwn. Frederick Kanga mwakilishi kutoka Exim Bank akisalimiana na mwanaDiaspora aliyetembelea meza hiyo kujaribu kupata mawili matatu.
WanaDiaspora wakipata mawasiliano na kuuliza maswali kwa makampuni yaliohudhuria Career Africa jijini New York. 

kwa picha zaidi Bofya Hapa

No comments:

Post a Comment