Monday, February 23, 2015

Jumuiya ya Tanzania Houston Community (THC) yapata Executive Committee Mpya


Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston, TX jioni ya jana katika ukumbi wa Community uliopo katika makutano ya barabara za Bissonnet na Kirkwood ilifanya uchaguzi wa Executive Committee (EC) na kupata wajumbe 7 waliongia katika kamati hiyo. Kinyang'anyiro hicho kilijumuisha wanajumuiya 8 waliojitokeza kuomba kuchaguliwa katika nafasi 7 zilizokuwepo.

Matokeo ya kura yaliwachagua wafuatao kuingia kwenye EC:

  1. MR. EMMANUEL C. EMMANUEL
  2. MR. LENNY MANGARA
  3. MRS. HILDA AFUTU
  4. MR. ANTHONY RUGIMBANA 
  5. MRS. REHEMA MAJOLLO
  6. MR. NEVILLE RUGAIMUKAMU
  7. MR.HANS MNGWAMBA


Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya hiyo ndugu DAVID MREMA hakupata kura za kutosha kuingia kwenye EC. Blog  hii inawapa hongera wote waliochaguliwa kuingia kwenye EC na kuwatakia mafanikio mema katika kufanya kazi ya kuipeleka Jumuiya yetu mbele kwenye mafanikio kwa kushirikiana timu ya uongozi inayoongozwa na Madam President NURU MAZORA.

Anthony Rugimbana akitoa machache baada ya kuchaguliwa

Wanajumuiya wakifuatilia yanayoendelea meza kuu
Wanajumuiya wakifuatilia yanayoendelea meza kuu
EC Teule toka kushoto : Rehema, Lenny, Hilda, Anthony, Emmanuel , Neville na Hans
Emmanuel akitoa shukurani kwa wapiga kura










Ndugu Fue

No comments:

Post a Comment