Monday, February 23, 2015

Mh.Sitta Ajibu Maswali ya Katiba Mpya kutoka kwa Wana-DMV

Mhe. Samwel Sitta amewasili nchini Marekani siku ya Jumapili Februari 22, 2015 na baadae jioni kukutana na Watanzania wa DMV na kuwafafanulia vifungu vya katiba iliyopendekezwa hasa kwenye swala la Serikali tatu na kueleza ni kwanini CCM ilipendelea serikali 2 na pia kufafanua swala la uraia pacha ambalo ndio kilio cha Diaspora na kuelezea kwa kina kifungu hicho ndani ya katiba iliyopendekezwa Mtanzania yeyote mwenye uraia wa nchi nyingine atakua na haki kama Mtanzania mwingine ikiwemo kumiliki ardhi na kutochukua VISA anaporudi nyumbani. Jambo ambalo hataruhusiwa ni kupiga kura au kugombea uongozi katika maswala ya siasa.

Baada ya maelezo marefu na yenye ufasaha ya katiba iliyopendekezwa, Mhe. Samwel Sitta pia aligusia shughuli za Wizara yake na mipango anayotarajia kuifanya ikiwemo kuimarisha Reli ya kati, viwanja vya ndege, Mwanza, Mbeya na Musoma na baadae kulikua maswali na majibu ambayo watu wengi walionekana kuridhishwa na majibu mazuri na yaliyowafumbua macho wanadiaspora huku Mhe. Samwel Sitta akisisitiza kwa wasaidizi wake wawe wakitoa maelezo ya kina kwa Diaspora  ili wasiwe nyuma na nyumbani. AUDIO ya mkutano wote yakiwemo maswali na majibu tutawawekea kesho msikie nini kimezungumuzia kwa wale ambao hawakubahatika kuhudhuria mkutano huo wakiwemo Watanzania wa majimbo mwengine. na wengine waliopo nje ya Tanzania.

Mwasho Mhe. Samwel Sitta alimshukuru dada Loveness Mamuya kwa kuwasiliana na ofisi yake na kuja na wazo la yeye kuja kufafanua vifungu vya katiba iliyopendekezwea,
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta (kati) akiambatana na mwenyeji wake Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula kuingia kwenye ukumbi wa Tabeer uliopo Hyattsville, Maryland nchini Marekani. 
Mhe. JOhn Sitta akiwa na mwenyeji wake Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula, Mbunge wa viti maalum CHADEMA Mhe. Leticia Nyerere pamoja na mmoja katika msafala wa Mhe.Sitta wakiwa wamesimsma kwa ajili ya wimbo wa Taifa.
WanaDMV wakiimba wimbo wa Taifa mara tu baada ya mgeni rasmi kuingia ukumbini.
Mchungaji John Mbatta akiongea machache na kumshukuru Mhe. Samwel Sitta kuja kuifafanua katiba iliyopendekezwa kwa wanaDiaspora.
Rais wa DMV Bw. Iddi Sandaly akitoa shukurani zake kwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta kwa kukubali kwake kuzungumuzia katiba iliyopendekezwa na kuitolea ufafanuzi.
Mhe. Liberata Mulamula akiwashukuru wanaDMV kwa kujitokeza kwa wingi.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta akisoma vifungu kwenye katiba iliyopendekezwa na kuvitolea ufafanuzi. Wengine katika picha toka kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula, Rais wa Jumuiya DMV Bwn. Iddi Sandaly na Mbunge viti maaluum CHADEMA Mhe. Leticia Nyerere.
WanaDMV wakifuatilia mkutano.
Mhe. Samwel Sitta akiongea na mwenyeji wake jambo Mhe. Liberata Mulamula.
Mhe. Samwel Sitta akiongea  jambo na mbunge wa viti maalum CHADEMA Mhe. Leticia Nyerere.
Benja Mwaipaja akimpongeza Mhe. Samwel Sitta baada ya kujibia maswali yake kwa ufasaha ikiwemo kama nayeye ataingia kwenye kinyang'anyiro cha urais na Mhe. kujibu inategemea na wananchi wakijitokeza kumshawishi na Benja kunyanyuka na kumpongeza na huku akisema nimekuotea ndoto tayari Mheshimiwa  huku wanaDMV wakivunjika mbavu kutokana na kitendo cha Benja kumfagilia Mhe. Samwel Sitta. 
Kwa picha zaidi bofya Bofys HAPA

No comments:

Post a Comment