Aliyekuwa muomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameenguliwa, Edward Lowassa akiwasili kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM kuhudhuria kikao cha NEC. |
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Mzee Msidai akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho cha NEC |
Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, wa CCM, Zakhia Meghji akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini |
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Steven Wasira akifuatwa na Waandishi wakati akiingia ukumbini |
Muomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Bernard Membe ambaye amefanikiwa kuingia tano bora, akizungumza na waandishi kabla ya kuingia ukumbini kwenye kikao hicho leo |
Muomba kuteuliwa kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, ambaye ameingia tano bora, John Magufuli, akimsikiliza kwa makini mmoja wa wajumbe wa NEC, aliyekuwa akimnong'oneza jambo kabla ya kuingia ukumbini |
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Januari Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora waliokuwa nje ya ukumbi wakati wa kikao hicho |
Wakuu wa vyombo vya habari vya CCM, Angel Akilimali (Uhuru FM) na Ramadhani Mkoma (Uhuru Publications Ltd) |
Muomba ridhaa ya CCM kuwania Urais Bernard Membe akiwasalimia wajumbe ukumbini pengine kuomba kura zao kabla ya kuanza kikao hicho
Waomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, ambao wamefanikiwa kuingia tano bora Bernard Membe na Dk. Asha Rose Migiro wakisalimiana ukumbini wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Samwel Sitta ambaye pia aliomba nafasi hiyo lakini hakuingia tano bora
Aliyekuwa muomba kuteuliwa na CCM kuwania Urais, Lazaro Nyalandu ambaye hakuingia tano bora, akizungumza na Adam Malima
Wajumbe wakiwa ukumbini
"Usijai kaka" Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM kuwania Urais, Mwiguku Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.
"Usijai kaka" Katibu wa NEC, Iikadi na Uenezi Nape Nnauye akimfariji aliyekuwa muomba rudhaa ya CCM kuwania Urais, Mwiguku Nchemba, ambaye hakuingia tano bora.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Edward Lowassa ambaye hakpita tano bora, wakati wa kikao hicho.
"Naomba kura yako Ndugu yangu" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho.
"Naomba kura yako Ndugu yangu" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho
"Naomba kura yako Ndugu yangu, tena napiga magoti" Bernard Membe ambaye amepitishwa na Kamati Kuu kuingia tano bora akimsalimia Edward Lowassa ambaye amekosa kuingia tano bora, wakati wa kikao hicho
January Makamba ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa wakati wa kikao hicho cha NEC
Membe na Januari Makamba wakisalimiana ukumbini
Baadhi ya wajumbe ukumbini
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mzee Sitta wakati wa kikao hicho cha NEC
Dk. Asha-Rose Migiro ambaye amefanikiwa kuingia tano bora akimsalimia Lowassa na kumuomba kura wakati wa kikao hicho cha NEC leo
Baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti wakiwa kwenye kikao hicho
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kikao hicho cha NEC
Ulizni ukiwa umeimarishwa katika jengo la White House baada ya baadhi ya walioomba ridhaa ya CCM kuwania urais na kutoingia tano bora, kudaiwa kuandaa fujo wakati wa kikao hicho cha NEC. Picha zote na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment