Thursday, November 5, 2015

MAWAZIRI WAAGIZWA KUREJESHA IKULU MAGARI YA SERIKALI LEO


Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, amewaagiza Mawaziri na Naibu Mawaziri leo kurudisha magari ya serikali baada ya Rais Mteule, Dk. John Magufuli kuapishwa kwa kuwa ndiyo siku yao ya ukomo wa uongozi.
Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Balozi Sefue alisema baada ya Bendera ya Rais kuteremshwa na kabla Bendera ya Rais mpya kupandishwa, magari ya mawaziri na Naibu Mawaziri, yatabadilishwa namba kwa kuondoa herufi ya cheo chake (W au NW) na kurejeshwa kwenye namba za serikali (ST).

Balozi Sefue alisema baada ya shughuli hiyo, magari hayo yatawarudisha nyumbani mawaziri na naibu Mawaziri waliomaliza muda wao na kurejeshwa Ikulu tayari kwa ajili ya kupewa mawaziri wapya watakaoteuliwa. 

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment