Friday, December 11, 2015

BALOZI WILSON MASILINGI AFANYA MCHAPALO WA KUJITAMBULISHA


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto) na mkewe Marystella Masilingi (wanne toka kushoto) wakiwakaribisha Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Marekani kwenye mchapalo ulioandaliwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya kujitambulisha kwao wakiwemo viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania nchini Marekani, viongozi wa Dini, DICOTA na vyama vya siasa siku ya Alhamisi Desemba 10, 2015 kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo mtaa wa 22 jijini Washington, DC. Kulia ni Afisa Ubalozi Bi. Swahiba Mdeme. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akisalimiana na Ben Kazora mmoja ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas mara tu alipowasili kwenye jengo la Ubalozi kuhudhuria mchapalo wa kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Wilson Masilingi, watatu toka kushoto ni mkewe Marystella Masilingi na kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme.
Afisa Suleiman Saleh akiwa kama mshereheshaji wa mchapalo huo akiwawakaribisha wageni na baadae kumkaribisha Afisa Swahiba Mdeme kwa ajili ya kumkaribisha Balozi Wilson Masilingi.
 
Afisa Swahiba Mdeme akiongea machache huku akisoma wasifu wa Mhe. Wilson Masilingi na baadae kumkaribisha Balozi kwa ajili ya kujitambulisha kwa wageni wake.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akijitambulisha kwa Waheshimiwa Mabalozi na viongozi wa Jumuiya za Watanzania nchini Marekani kwenye mchapalo ulioandaliwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya kujitambulisha kwao uliofanyika siku ya Alhamisi Desemba 10, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Waheshimiwa Mabalozi, viongozi wa Jumuiya za Watznania nchini Marekani wakimsikiliza Mhe. Balozi Wilson Masilingi.
Baadhi ya Vingozi wa Jumuiya za Watanzania nchini Marekani kutoka kushoto ni Bwn. Hajji Kassim Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Lunda Asmani kiongozi wa DICOTA, Bwn. Ben Kazora Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas na Bwn. Iddi Sandaly Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi (watatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na jumuiya ya Watanzania DMV na viongozi wa TAMCO. Kutoka kushoto ni Said Mwamende katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV na mmwanachama wa CHADEMA, Shamis kiongozi wa TAMCO na mwanachama wa CUF na ZADIA, Salma Moshi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM DMV, Ali Mohammed Mwenyekiti wa TAMCO na Bernadeta Kaiza Katibu msaidizi wa Jumuiya ya Wanzania DMV.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

No comments:

Post a Comment