Monday, April 25, 2016

Nico Njohole Awasili Houston Tayari kwa Mpambano wa SIMBA na YANGA, DALLAS

Nico Njohole (kati) akiwa kwenye harambee ya Andrew Sanga iliyofanyika 
Jumamosi April 23, 2016 jijini Houston, Texas. 
Picha na Cassius Pambamaji mwakilishi wa Vijimambo Houston
Renatus Njohole akiwa kwenye moja ya mechi na timu ya daraja la tatu FC Bavois nchini Switzerland
Na Vijimambo, Dallas, Texas

Mchezaji Nico Njohole ambaye amekuja maalum kwenye DICOTA na mechi ya Simba na Yanga itakayochezewa kwa mara ya kwanza Dallas, Texas. Mchezaji huyo anayetokea Uingereza aliwasili Houston, Texas, siku ya Alhamisi April 21, 2016 na siku ya Jumamosi alishiriki harambee ya Mtanzania aliyekufa kwa ajali ya kupigwa raisasi huko Houston, Texas, marehemu Andrew Sanga.

Renatus Njohole atawasili siku ya Jumamtano Houston, Texas na kama ilivyoripotiwa hapa awali mpambano huu wa Simba na Yanga utawashirikisha kwa mara ya kwanza wachezaji wawili waliowahi kwa nyakati tofauti kuichezea Clab ya Simba. Simba na Yanga kuchezwa nje ya DC itakua mara ya tatu, mara ya kwanza ilikua Columbus, Ohio, na mara ya pili ilichezewa Houston, Texas Safari hii mpambano utakaochezwa Dallas katika kiwanja cha Hufthines Recreation Center ambacho anuani yake ni 200 N Piano Road, Richardson, TX 75081. 

Mapambano huu utakua wa wazi kwa mashabiki na wachezaji kujumuika pamoja na kuandika historia ambako kwa mara ya kwanza utaandika historia mpya ya kuchezwa na wachezaji wawili waliowahi kuichezea Club ya Simba. Michezo mingine iyakayokuwepo ni mpirsa wa kikapu na mpira wa wavu ikienda sambamba na nyama choma.

Mechi hii inayosubiliwa kwa hamu ni sehemu ya burudani itakayokuwepo kwenye kongamano la DICOTA ambalo mwaka huu linafanyika Dallas, Texas kuanzia April 28, mpaka May 1, 2016. Mashabiki na wachezaji wa pande zote wameanza kutupiana vijembe huku mashabiki wa Simba wakifurahia ujio wa Renatus Njohole na kaka yake Nico kuja kutia nguvu timu hiyo ambayo mechi nyingi za Simba na Yanga ughaibuni huishia kupata kipigo kutoka kwa mahasimu wao.

Timu ya Simba ughaibuni ina historia nzuri inapocheza nje ya DC, mara zote imeibuka mshindi.

Huu utakua mpambano wa pili wa Simba na Yanga kugombea kombe la DICOTA mara ya kwanza timu hizi zilikutana kwenye kongamano la DICOTA lililofanyika Washington, DC mwaka 2011 na kongamano hilo Rais mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete ndiye aliyekua mgeni rasmi kwenye kongamano hilo..

No comments:

Post a Comment