Monday, April 25, 2016

CLOUDS Media Group yamtembelea Balozi Manongi jijini New York

Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe.Balozi Tuvako Manongi akimkaribisha Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga nyumbani kwake siku ya Jumamosi April 23, 2016 siku mkurugenzi huyo alipotembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakzi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika Las Vegas, nchini Marekani. Picha na Vijimambo New York.

Mhe. Balozi Tovako Manongi akiwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn, Joseph Kusaga (hayupo picha) siku ya Jumamosi April 23, 2016 siku mkurugenzi huyo alipotembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakazi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika Las Vegas, nchini Marekani.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwn. Joseph Kusaga akitambulisha timu yake kwa
Mhe. Balozi Manongi.

Mhe. Balozi mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn. Joseph Kusaga
.
Mkurugenzi wa Clouds Medea Group, Bwn. Joseph Kusaga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Manongi na mkewe.

Timu nzima ya Clouds Medea Group wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi na mkewe, kutoka kushoto ni Saleh Mohamed, Daudi Lembuya, Dj Venture, Mhe. Balozi  Manongi, Mgurugenzi Joseph Kusaga, mama Manongi, Dj Peter Moe na Jackson Joseph.

Kushoto ni Brightus Titus, Getrude Clement na NY Ebra wakiwa katika picha ya pamoja
.


No comments:

Post a Comment