Tuesday, May 24, 2016

WANA-HOUSTON WAKUTANA NA LEAD DETECTIVE WA KESI YA MAUAJI YA ANDREW SANGA

Siku ya Jumamosi iliyopita (tarehe 21-Mei-2016) idadi kubwa ya wanajumuiya ya Watanzania wanaoishi katika jiji la Houston, Texas na vitongoji vyake walikutana na Bw. Todd Tyler ambaye ni Lead Detective wa kesi ya mauaji ya mpendwa wao Andrew Sanga aliyeuawa kwa kupigwa risasi takribani wiki tatu zilizopita na watu wasiojulikana . Sababu kubwa ya mkutano huo uliosimamiwa na uongozi wa Jumuiya wakiongozwa na Rais wa THC Bw.Daudi Mayocha ilikuwa ni kutaka kujua hatua ambayo kesi hiyo limefikia na kama wanajumuiya wanaweza kutoa mchango wowote katika kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa\watuhumiwa wa mauaji hayo.

Kwa kifupi mpelelezi huyo Bw.Todd Tyler alisema bado wanaendelea na uchunguzi na hadi siku hiyo alipokutana na wanajumuiya walikuwa bado hawajamkamata mtu yoyote kuhusiana na mauaji kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha hadi sasa. Bw.Tyler aliomba ushirikiano wa mtu yoyote ambaye ana taarifa itakayopelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa/watuhumiwa. Pata picha za tukio hilo hapa chini.

Bwana Tyler akiwasili kwenye mkutano na kupokelewa na
 Rais wa THC Bw.Mayocha

Bwana Tyler akiwa na Bw.Mayocha na Katibu Mkuu wa THC Bw. Ndejembi 
Rais wa THC akifafanua jambo kwa Bw.Tyler

Bw.Tyler akipitia orodha ya maswali yaliyoandaliwa na wana Houston 
Sehemu ya wana Jumuiya
Wanajumuiya wakimsikiliza Bw. TylerNo comments:

Post a Comment