|
Dkt.Daniel Moses Kulola |
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani) yuko nchini Marekani kwa huduma ya kiroho tangu jumanne iliyopita Agosti 16,2016 ambapo alianza kuhudumu ijumaa Agost 19,2016 katika Kanisa la "Assemblies Of God Agape Church" lililopo Boston Marekani.
Huduma ya Mchungaji Dkt.Kulola inaendelea katika majimbo mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Texas (Dallas & Houston) na Arizona.
Aidha Mchungaji Kulola ametoa shukurani zake za dhati kwa familia yake, Kanisa la EAGT Lumala Mpya, ndugu, jamaa pamoja na marafiki kwa kuendelea kumuombea kwa huduma anayoifanya nchini Marekani ambapo watu wengi wanaokoka na kuponywa.
|
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akihudumu nchini Marekani. |
|
Picha ya pamoja baada ya huduma katika jimbo la Boston |
|
Mchungaji Kulola (katikati) na familia yake |
|
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola(kulia) |
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi
No comments:
Post a Comment