Saturday, August 27, 2016

TANZANIA HOUSTON COMM TEAM SAFARINI KUELEKEA ATLANTA LABOR DAY WEEKEND

Kikosi cha timu ya soccer ya Tanzania Houston Community maarufu kwa jina la DSQUAD wikiendi ya Labor Day kitakuwa mjini Atlanta, GA kupambama na kikosi cha TANZANITE FC katika mechi ya kumbukumbu ya mchezaji wao Marehemu Andrew Sanga aliyefariki takribani miezi minne iliyopita. Mechi hii ni maalumu kwa ajili ya kumuenzi marehemu Andrew ambaye enzi za uhai wake aliwahi kuishi katika miji hii mikubwa miwili ya Marekani ( Houston & Atlanta )
 
TANZANIA HOUSTON COMMUNITY - DSQUAD


TANZANITE FC - ATLANTA

Akizungumza na Blog hii Nahodha wa timu ya DSQUAD Bw. Alune Mwasabite alisema vijana wamejiandaa vizuri kwa mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi (09/03/2016) jioni katika viwanja vya Hammond Park, 705 Hammond Dr NE, Sandy Springs, GA 30328. Kikosi cha DSQUAD kinategemewa kuondoka Houston siku ya Ijumaa jioni na kufika Atlanta alfajiri ya jumamosi

No comments:

Post a Comment