Wednesday, August 31, 2016

MAMA WA MITINDO NA YASIN KAPUYA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE TAMASHA NCHINI MAREKANI

Taarifa mpya kwa wadau wa mitindo na fashion kwa vyombo vya habari inasema  Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin kutoka Tanzania anategemea kuiwakilisha Tanzania kwa kuonyesha mitindo yake katika jukwaa kubwa la biashara nchini Marekani katika mji mkuu wa Sacramento, California.


Tamasha hilo linalotambulika kama 'The African Trader Show' litafanyika kwa siku 3 kuanzia tarehe 2/9/2016 - 4/9/2016. Mbali na Asya pia Mr. Yasin Kapuya atawakilisha Tanzania kwa kutoa mada na kuonesha ufundi wa kazi zake katika onyesho hilo. Hivyo ndugu jamaa na marafiki na Watanzania wote kwa ujumla wanaoishi katika Jiji la Sacramento na miji mingine ya karibu tunaombwa kutoa ushirikiano wadhati kwa Wanzanzania hao.


No comments:

Post a Comment