Monday, August 22, 2016

TAASISI YA THE HOPE CAMPAIGN YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA CHAMAZI JIJINI DAR ES SALAAM

Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama (kushoto), akiwaelekeza maofisa wenzake kabla ya kwenda kukabidhi msaada huo.
Mizigo ikitolewa kwenye gari
                           Aman Issaya wa taasisi hiyo akiwa na kiroba cha sukari akielekea eneo la makabidhiano
Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama, akiwa amebeba kiroba cha sukari wakati taasisi hiyo ilipotoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temekie jijini Dar es Salaam leo.

Vifaa hivyo viwekwa sawa kabla ya kukabidhi.

Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Kituo hicho, msaada huo. Kulia ni Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama na Furaha Kapama.
Furaha Kapama (kushoto), akimkabidhi msaada Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Fred George. 

MwezeshajiMkuu wa Kampuni hiyo, John Amigo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili akiwa katika pozi.
Upendo Kapama akikabidhi msaada huo.
Thomas Anzuluni akimkabidhi Katibu wa kituo hicho, Fred George msaada wa mafuta ya kula.

Mwakilishi wa Taasisi ya The Hope Campaign, Stela Mpelo (kushoto), akiwakabidhi vifaa vya shule watoto Yatima wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Ofisa wa taasisi hiyo, Thomas Anzuluni na Katibu wa kituo hicho, Fred George.
Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), na Katibu Mkuu wa Kituo hicho wakiwa wameshika mipira iliyotolewa na taasisi hiyo kwa watoto wa kituo hicho.

Hapa ni kikosi kamili cha taasisi hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Ni pozi la kukata na shoka na vipeperushi mkononi.Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya The Hope Campaign imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada huo kituoni hapo Dar es Salaam leo asubuhi , Mratibu wa Taasisi hiyo Mpelo Kapama alisema msaada huo umelenga kuwasaidia watoto hao kwa ajili ya chakula na vifaa vya kusomea.

"Taasisi yetu kupitia kwa mwezeshaji  wetu mkuu John Amigo imejijengea utamaduni wa kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji kama watoto hao na kambi za ukimbizi na mara nyingi tumekuwa tukisaidia kituo hiki" alisema Kapama.

Katibu wa Kituo hicho cha Yatima, Fred George alisema ni muhimu kwa jamii kujitokeza kusaidia Yatima na kuwafariji kama ilivyofanya taasisi hiyo.

Alisema kituo hicho chenye watoto zaidi ya 150 kimekuwa na changamoto ya chakula, fedha za kuwalipa wafanyakazi pamoja na ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)No comments:

Post a Comment