Monday, August 22, 2016

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUTANGAZA HIFADHI ZAKE

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.

Tukio la kupatwa kwa jua linataraji kuonekana vizuri ukilinganisha na maeneo mengine Duniani katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani hapa,eneo ambalo liko jirani na Hifadhi za taifa za Ruaha, Kitulo na Katavi.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete alisema maandalizi kwa ajili ya kupokea wageni wanaotarajia kufika nchini kwa ajili ya tukio hilo ambalo limekuwa likitokea kwa nadra.“ Wataaam na wanasayansi wakitaifa na wakimataifa wathibitisha kuwa  eneo pekee ambalo tukio hilo litaonekana vizuri kuliko maeneo yote duniani ni Tanzania katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,eneo ambalo lina vivutio utalii vinavyopatikana katika hifadhi zetu za Katavi, Kitulo na Ruaha” alisema Shelutete .

“Shirika limejipanga kuhakikisha kuwa wageni wanoukuja kwa ajili ya tukio hilo pia wanapata fursa ya kuingia katika moja ya hifadhi zetu,niwaomba wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia nafasi
hii adhimu kukutana na wageni wanaokuja ili kuuza bidhaa zao za utalii” aliongeza Shelutete.

Naye mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Christopher Timbuka alisema kituo kikubwa ambacho kimethibitishwa kutumika kwa ajili ya watu kujionea vizuri tukio hilo ni katika eneo la Rujewa
wilaya ya Mbarali ambako maandalizi yote muhimu yamefanyika.

Kwa upande wake mhifadhi wa idara ya  utalii Tutindaga Mdoe alisema baada ya taarifa za tukio hilo
kuthibitishwa idadi ya wageni imeanza kuongezeka na kwamba wameandaa mahema na eneo la vyakula na vinywaji kwa wageni watakaofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Bonde la Ihefu lililopo katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Utafiti mdogo uliofanywa na Blog hii katika eneo hilo maarufu kwa kilimo cha mpunga umebaini asilimia kubwa ya nyumba za kulala wageni tayari zimejaa kwa tarehe ya tukio hilo.No comments:

Post a Comment