Tuesday, September 13, 2016

TANGAZO


Wapendwa,


Kama kuna mtu ana taarifa za huyu mtu hapa juu, naomba atoe taarifa rasmi kwenye dawati la Detective Matt Vendemio, Montgomery County Maryland Police, Patrol Investigation Unit 4th District , 2300 Randolph Road Wheaton, Maryland 20902 / 240-773-5500 (front desk).

Tunaomba msaada wenu, mjitokeze kwani hadi sasa ameshachukua pesa zaidi ya $50,000 toka kwa Watanzania wengi walioko Marekani na baadhi ya viongozi toka Tanzania. Tayari kuna Watanzania aliowatapeli wameshafungua mashitaka dhidi yake na uchunguzi unaendelea toka state mabalimbali hapa Marekani.

Jina lake la halali ni WILLBROD FRANK LUKAMILWA . Amekuwa anajitambulisha kwa watu kwa majina tofauti tofauti. Kwa sasa kuna records kuwa ameshajitambusha kwa wengi kama Padri John, Padri Frank, Doctor Frank wa Georgetown Hospital, Pediatrician wa The Children Place, Mwanafunzi wa PhD wa Catholic University, Steve, Frank. Frank Stockman na John. Pia amekuwa akitoa maelezo kuwa ni mtu wa nchi tofauti kama Senegal, South Africa, Kenya, Congo na Belgium wakati ni Mtanzania wa mkoa wa Kagera.

Ametumia maelezo ya watu na mitandao kupata pesa toka kwa watu wengi walioko nje na ndani ya USA. Namba za simu za mkononi ambazo ameshatumia siku za karibuni ni
202-446-7747 na 202-867-2691. Wilbrod alishashikwa mwaka huu June kwa utapeli pia, na bado anaendelea.


Tunaomba ushirikiano wenu wa hali na mali, hata kuwagundua ndugu zake walioko Tanzania. Ni mwenyeji wa Bukoba, mkoa wa Kagera, Tanzania.

Huyu mtu ni hatari sana usimpe nafasi ya kuwasiliana na wewe kwani anatumia njia nyingi sana za utapeli (scamming schemes), tafadhali toa taarifa zako kama ni mmojawapo wa watu waliokwisha tapeliwa na huyu mtu.

http://www.nbcwashington.com/news/local/Police-Recognize-Arrest-Man-Right-After-Handing-Out-Wanted-Ads-383310751.html )

No comments:

Post a Comment