Sunday, September 27, 2020

GAME DAY SOCCER LEAGUE: DSQUAD YAICHAPA FUTSAL FC 2-1

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD jioni ya leo katika viwanja vya Alvin Community College iliyaanza kwa kishindo mashindano ya GAME DAY SOCCER LEAGUE2020 kwa kuichapa timu ya FUTSAL FC mabao 2-1. Magoli ya DSQUAD yalifungwa na winga wake machachari Iluta Shabani katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi murua kutoka kwa mkongwe Peter Bategeki. Baada ya kosakosa nyingi za DSQUAD timu ya Futsal walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Amigo Espinoza aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa Hermano Gonzalez katika dakika ya 75. 

Wakati kila mtu akitegemea mechi itaisha suluhu nahodha wa DSQUAD Rahim Sterling Chomba alifunga bao la pili kwa mkwaju wa adhabu ulioenda moja kwa moja nyavuni baada ya kiungo msumbufu Abahenya Ngolo kufanyiwa madhambi umbali wa mita 35 kuto golini mwa Futsal. 

Mashindano haya yataendelea wiki ijayo katika viwanja hivi vya Alvin Community College. Nyote mnakaribishwa.
No comments:

Post a Comment