Monday, October 5, 2020

GAME DAY SOCCER LEAGUE: DSQUAD YAICHAPA PEARLAND SC 4-2

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD jioni ya leo katika viwanja vya Hickory Slough Sportsplex vilivyoko Pearland iliendeleza vipigo kwenye mashindano ya GAME DAY SOCCER LEAGUE2020 kwa kuichapa timu ya PEARLAND SC jumla ya mabao 4-2. Magoli ya DSQUAD yalifungwa na mshambuliaji wake machachari Tom Juma aliyepachika mabao mawili katika dakika ya 35 na 75. Mabao mengine yalifungwa na winga tereza Iluta Pepe Shabani dk ya 55 na bao la nne likiwekwa nyavuni na nyota wa mchezo wa leo Amini Ceballos Msisi katika dakika ya 82 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Pearland SC. Magoli ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Juaquin Rodrigo yalikuwa kama kifuta machozi kwa Pearland SC 

Mashindano haya yataendelea wiki ijayo katika viwanja vya Alvin Community College. Nyote mnakaribishwa.

                       













































































































































































































































































































































































No comments:

Post a Comment