Sunday, October 18, 2020

GAME DAY SOCCER LEAGUE: DSQUAD YAICHAPA GUERREROS FC 4-2

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD jioni ya leo katika viwanja vya Alvin Community College vilivyoko Alvin, Texas iliendeleza vipigo kwenye mashindano ya GAME DAY SOCCER LEAGUE2020 kwa kuichapa timu ya GUERREROS FC jumla ya mabao 4-2 na kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 12. Magoli ya DSQUAD yalifungwa na mshambuliaji wake machachari Jason Esson katika dakika ya 22 kabla ya mlinzi Mudhihir Said kufunga bao la pili katika dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya golikipa wa Guerreros FC Wilmer Ramirez kumfanyia madhambi kiungo Amini Ceballos Msisi na muamuzi kuamuru mkwaju wa penati upigwe. 
Dsquad waliendelea kushambulia kama nyuki na kujipatia bao la tatu katika dakika ya 44 lililofungwa na winga wa kulia Ramadhan Ngolo baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Jason Esson. 
Kipindi cha pili kilikuwa na mashambulizi zaidi ya Dsquad ambao walipoteza nafasi nyingi za kufunga hadi dakika ya 78 pale winga machachari Iluta Shabaan alipomimina krosi maridadi iliyomaliziwa nyavuni na chipukizi Said Mvano.

Mashindano haya yataendelea wiki ijayo katika viwanja vya Alvin Community College. Nyote mnakaribishwa.

No comments:

Post a Comment