Monday, December 7, 2020

GAME DAY SOCCER LEAGUE PLAYOFFS: DSQUAD YAIBAMIZA FC BLAZE 4-2

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD jioni ya leo tena katika viwanja vya Alvin Community College vilivyoko Alvin, Texas iliendeleza vichapo baada ya kuikung'uta bila huruma FC BLAZE kwa jumla ya mabao 4-2 katika mashindano ya GAME DAY SOCCER LEAGUE2020 .

Mechi hiyo ya kwanza ya PLAYOFFS ilikuwa ni kali na ya kusisimua huku DSQUAD ikiwatumia wachezaji wake vijana waliocheza kwa mara ya kwanza kama Francois, Adrian, Antonio, Edward etc.

DSQUAD ilijipatia magoli yake kupitia kwa mshambuliaji Peter Dotto, Adrian, Iluta Shabani "Mbappe" na Ramadhan Ngolo "Aubameyang".

No comments:

Post a Comment