Sunday, November 22, 2020

GAME DAY SOCCER LEAGUE: DSQUAD YAIBAMIZA SoK FC 6-0

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD jioni ya leo tena katika viwanja vya Alvin Community College vilivyoko Alvin, Texas imeichapa timu ya SoK FC kwa mabao 6-0 kwenye mashindano ya GAME DAY SOCCER LEAGUE2020 .

Mechi hiyo iliyokuwa ya kumaliza msimu wa kawaida kabla ya kuanza kwa PLAYOFFS tarehe 06 December ilikuwa ngumu lakini DSQUAD walikuja wakiwa wamejiandaa kuondoka na ushindi mkubwa.

DSQUAD ilijipatia magoli yake kupitia kwa mshambulia Jason Esson "The Jamaican" (2), Iluta Shabani "Mbappe" (2), Ramadhan Ngolo "Aubameyang" na Abubakar Mudhihir "Wan Bissaka".

Ngome ya SoK FC iliyokuwa chini ya mabeki Izechukwu Amokachi na Roman Cuardado haikuweza kufanya chochote kuwazuia washambuliaji wenye uchu wa DSQUAD.

No comments:

Post a Comment