Saturday, January 2, 2021

GAME DAY SOCCER LEAGUE PLAYOFFS: DSQUAD YAIBAMIZA ATHENRY 3-2 NA KUKARIBIA KUBEBA UBINGWA

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD jioni ya leo tena katika viwanja vya Pearland Hickory Slough, Texas iliendeleza vichapo baada ya kuikung'uta bila huruma ATHENRY kwa jumla ya mabao 3-2 katika mashindano ya GAMEDAY SOCCER LEAGUE2020.

Mechi hiyo ya ngumu ya PLAYOFFS ilikuwa ni kali na ya kusisimua. DSQUAD ilihitaji ushindi ili kujisogeza karibu na ubingwa. Ikiwatumia wachezaji wake vijana DSQUAD ilijipatia goli la kwanza katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo mkata umeme Antonio Kamengele "Antoninho" aliyepiga shuti kali la umbali wa mita 40 na kumuacha golikipa Terry Richards wa Athenry akiwa hana la kufanya.

DSQUAD ilijipatia magoli yake mengine mawili katika kipindi cha pili kupitia kwa washambuliaji wake hatari Peter Dotto "Rashford" na Iluta Shabani "Mbappe" . Mechi ya mwisho itakuwa kesho saa 7 mchana dhidi ya SE United.GOOOOOOOALLLLLLLLNo comments:

Post a Comment