Sunday, January 3, 2021

GAME DAY SOCCER LEAGUE FINALS: DSQUAD YATWAA UBINGWA

Timu ya Tanzania Houston Community maarufu kama DSQUAD mchana wa leo katika viwanja vya Pearland Hickory Slough, Texas imetangazwa rasmi kuwa MABINGWA wapya wa GAMEDAY SOCCER LEAGUE2020. DSQUAD wakiwa tayari na uhakika wa ubingwa baada ya ushindi wa jana dhidi ya ATHENRY walifika uwanjani lakini wapinzani wao SE United wakaingia mitini na hivyo kuwafanya rasmi kutawazwa kama mabingwa wapya. Huu ni ubingwa wa kwanza baada ya miaka takribani 18 kwa timu hii ya Watanzania wanaoishi katika jiji hili la Houston, Texas.

Kwa ushindi huu DSQUAD imenyakua kikombe na kupanda rasmi kwenye Champions League ambayo inaanza rasmi msimu mpya wikiendi ijayo.

No comments:

Post a Comment