Picha juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akitoa neno la shukurani kwa kamati ya miji dada Durham na Arusha kwa kumkaribisha kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo katika kuendelezamashirikiano kati ya nchi za Tanzania na Marekani katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo uwekezaji. Picha na Vijimambo Blog |
Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya miji dada Durham na Arusha (SCD) Bi. Ronda Pierce akieleza historia ya kamati ya miji dada na mashirikiano yao na mji wa Arusha na Durham tangu mashirikiano hayo yalipoanzishwa. |
Meya wa mji wa Durham anaemaliza muda wake Bw. Steve Schewel akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza na kuelezea mashirikiano ya mji wa Durham na Arusha na safari yake nchini Tanzania hususani kwenye mji wa Arusha. |
Rais wa miji dada ya Durham na Arusha (SCD) Bwn.Tom Harris akitoa salamu kwa Mhe. Balozi kutoka kwa Kamati ya miji dada ya Durham na Arusha (SCD) |
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya miji ya Durham na Arusha Bi.Gwendolyn Bookman akitambulisha Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza kwa kusoma wasifu wake na baadae kumkaribisha kuongea na hadhara iliyojumuika pamoja na kamati ya miji dada ya Durham na Arusha katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara |
Picha juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Meya wa Durham anayemaliza muda wake akiwemo Rais wa SCD (miji dada ya Durham na Arusha) na wadau wengine kwenye maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. |
Meya mteule wa Durham Bi. Elaine Neel akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza |
Meya wa zamani wa mji wa Durhan Mhe.William Bell akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza |
Kansela wa Chuo Kikuu Cha NCCU ( North Carolina Central University Bwn. Johnson Akinleye akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza |
Mwenyekiti wa Jumuiya ya waTanzania North Carolina Scolastica akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza |
Kushoto ni Afisa Ubalozi Bi Jean Msabila na Mkuu wa Utawala na Fedha Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia jambo kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyokuwa yameandaliwa na Kamati ya Miji dada ya Durhan na Arusha katika Chuo Kikuu cha NCCU (North Carolina Central University) siku ya Jumapili Disemba 5, 2021. |
Picha juu na chini wageni waalikwa wakiwemo wadau mbalimbali wakifuatilia maadhimisho hayo. |
Picha juu na chini wadau mbalimbali wakiuliza maswali wakiwemo wawekezaji wanaowekeza nchini Tanzania wanaotokea North Carolina. |
Picha juu na chini wageni waalikwa wakiwemo wadau wakibadilishana mawili matatu kabla ya maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara kuanza. |
No comments:
Post a Comment