Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akiongea jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mhe. Peter Lord anayeshughulikia maswala ya Afrika Mashariki, Sudan na Sudan ya Kusini |
Picha juu na chini ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akisoma hotuba yake kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara siku ya Alhamisi Disemba 9 |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akipongezwa kwa hotuba nzuri na Balozi wa Rwanda Mhe. Mathilde Mukantabana |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mhe. Peter Lord anayeshughulikia naswala ya Afrika Mashariki, Sudan na Sudan ya Kusini akisoma hotuba yake akipongeza mashirikiano katika nyanjambalimbali kati ya Marekani na Tanzania na kuipongeza Tanzania kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru. |
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mhe. Peter Lord anayeshughulikia naswala ya Afrika Mashariki, Sudan na Sudan ya Kusini kwa hotuba yake |
Picha juu na chini Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akisamiliana na wageni mbalimbali wakiwemo waheshimiwa Mabalozi na Waambata wa Jeshi wa Balozi zao. |
Mshereheshaji Bi Tuma akisherehesha maadhimisho hayo. |
Nyimbo za Taifa Marekani na Tanzania zikipigwa kuashiria ufunguzi rasmi wa Maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. |
Msanii wa kikundi cha Tanzanite African Acrobatics kutoka Miami akiwatambulisha wasanii wenzake kwenye kundi hilo walipokua sehemu ya kusherehesha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara uliofanyika siku ya Alhamisi Disemba 9, 2021 katika hotel ya Washington Marriott, Washington, DC. Kundi lina wasanii wanne Matiga Kobs, Emmanuel Mbonde, Faraji Ngingite na Sadick Shabani |
No comments:
Post a Comment