Sunday, July 24, 2022

IMBA TOGETHER YAITIKISA WINSTON SALEM, NORTH CAROLINA NCHINI MAREKANI

Anna Simtaji, mwanzilishi wa IMBA Together na mmiliki wa AJS, kampuni iliyodhamini tamasha lote kwa ukubwa wake Tamasha funga kazi ambalo halijawahi tokea lililojumuisha watu wa mataifa mbalimbali kutoka majimbo karibu yote Marekani na wengine kutoka Tanzania, wasanii wakubwa wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, Kenya na hapa Marekani. Tamasha lilifanyika siku ya Jumamosi July 23, 2022, Winston Salem, North Carolina, nchini Marekani. Picha na Vijimambo Blog.
Anna Simtaji akiongea machache na kuwashukuru wote kwa kujumuika pamoja katika kumtukuza Mungu na baadae kumkaribisha msatahiki Mayor wa Winston Salem kuja kuongea machache na hadhara iliyokuja kushuhudia tamasha kubwa la Gospel ambalo halijawahi kutokea nchini Marekani.
Mgeni rasmi Mstahiki Mayor wa Winston Salem, North Carolina Mhe. Allen Joines akiongea machache katika kufungua tamasha kubwa la Gospel lililoenda sambamba na ufahamu wa watoto wenye usonji. Tamasha hili kubwa lilifanyika katika ukumbi wa Millennium Center siku ya Jumamosi July 23, 2022 na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka majimbo karibu yote hapa Marekani na Tanzania.
Kulia nio mshereheshaji aliyesherehesha harusi ya Masanja Mkandamizaji akiwakaribisha Masanja (kati) na Kristin (kushoto) ambao ndio walionogesha tamasha hilo kubwa la Gospel la aina yake kama washereheshaji na kufanikisha sana, mande yao ua ueMC walilishambulia jukwaa kisawa sawa.
Kristin na Masanja wakiwa kazini.
Bofya soma zaidi, Kwa picha zaidi na Video nzima ya Tamasha wakiwemo wasaani wakubwa walionogesha tamasha la IMBA Together.
Picha juu na chini ni Msanii John akifungua pazia akionyesha ukomavu wake usiku wa Tamasha la IMBA Together na kuwakuna sana wadau wa Gospel waliojumuika pamoja kwenye tamasha hilo.
Msanii Edna Matinde akilishambulia jukwaa kwa hisia kali katika kunogesha tamasha kubwa la IMBA Together.
Msanii Leonard akionyesha ubora wake wa kupiga gitaa la nyuzi 12 huku akiimbo nyimbo za kumsifuna Mungu.
Msanii Collins akiwasha moto na Ritungu yake.
Msanii Gloria Muliro kutoka Kenya na New York akifanya kile alichozoea siku zote.
Kundi la Kelly and Matt ktoka Marekani wakitumbuiza Tamasha la IMBA Together.
Picha juu na chini ni msanii Dr. Ipyana Tanzania pamoja na kumpoteza baba yake mzazi saa chache kabla hajapanda jukwaani, alimtukuza Mungu kwa kuimba katika tamasha kubwa la IMBA Together lililofanyika siku ya Jumamosi July 23, 2022 Winston Salem, North Carolina, nchini Marekani.
Picha juu na chini ni msanii Joel Lwanga kupka Tanzania akiwasha moto usiku wa IMBA Together, Winston Salem, North Carolina.
Picha juu na chini ni msanii Goodluck Gozbert akipagawisha jukwaa akiwa pamoja na kundi la Swahili Dancers kutoka Minnesota.
Picha juu na chini ni msanii Rehema Simfukwe kutoka Tanzania naye alikuwepo kwenye Tamasha la IMBA Together.
Picha juu na chini ni msanii Boaz Danken akifunga pazia IMBA Together ikiandika historia kubwa ya Gospel nchini Marekani.
Picha juu na chini ni kundi la Swahili Dancers kutoka Minnesota wakinogesha na kushambulia Jukwaa lMBA Together.
Mchungaji wa Swahili Church kutoka Dallas, Absalom Nasuwa atoa neno la Bwana Mungu wetu usiku wa IMBA Together.
Chini ni Video ya Tamasha zima la IMBA Together

No comments:

Post a Comment