Friday, July 22, 2022

WATANZANIA KATIKA MECHI YA MANCHESTER CITY VS CLUB AMERICA ILIYOFANYIKA JIJINI HOUSTON JIMBONI TEXAS

 Siku ya jana tarehe 20/07/2022 katika dimba la NRG Stadium lililoko katika jiji la Houston , Texas nchini Marekani kulifanyika pambano la kukata na shoka kati ya mabingwa wa England klabu ya Manchester City dhidi ya miamba ya soka Club America kutoka nchini Mexico. Pambano hilo lilihudhuriwa na mashabiki zaidi ya 61,000 miongoni mwao wakiwemo Watanzania wanaoishi Jijini Houston na miji mingine ya karibu. Mwisho wa mpambano huo Man City waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwa mabao yaliyofungwa na kiungo wao mahiri kutoka Belgium Kevin De Bruyne. Pata picha za tukio hilo


No comments:

Post a Comment