Monday, July 10, 2023

MHE. BALOZI DKT. ELSIE KANZA AONGOZA SIKU YA MAADHIMISHO YA LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI JIJINI WASHINGTON DC

Bendera zikiwakilisha mataifa ya Afrika ndani ya jengo la Ubalozi wa African Union
Washington, DC, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani, Ijumaa July 7, 2023 na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani na Mexico Mhe. Dkt. Elsie Kanza (hayuopo pichani ) aliongoza maadhimisho hayo. yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili wakiwemo Waheshimiwa
Mabalozi waalikwa pamoja na mwenyeji wao Balozi wa African Union nchini
Marekani Mhe. Hilda Suka Mafudze. Picha na Vijimambo Blog

Wa tatu toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na
Mexico Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Mabalozi
waalikwa. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Eswatini Mhe. Kennedy Fitzgerald Groening
akifuatiwa na Balozi wa Ukraine Mhe. Oksana Markarova na wa mwisho kulia ni
Balozi wa Kenya Mhe. Lazarus O. Amayo

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Elsie Kanza akiongoza
maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijumaa
 July 7, 2023 katika jengo la Ubalozi la African Union Washington, DC.

Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe. Hilda Suka Mafudze (kulia) akitoa hotuba ya
ufunguzi siku ya maadhimisho ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika katika jengo la
Ubalozi la African Union Washington, DC. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini
Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akifuatilia hotuba hiyo. 

Watatu toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza
akiwa na wageni wake waheshimiwa Mabalozi walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya
 siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya
Ijumaa July 7, 2023. Washington, DC.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akiwa na wageni wake waheshimiwa Mabalozi walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili
Duniani yaliyofanyika siku ya Ijumaa July 7, 2023.

Wadau wa lugha ya Kiswahili wakifuatilia maadhimisho hayo yaliyofanyika siku ya
 Ijumaa July 7, 2023 katika jengo la Ubalozi la African Union lililopo
Washington, DC nchini Marekani.


Jopo la wadau wa Kiswahili wakijiandaa kuelezea jinsi wanavyoipambania lugha ya
Kiswahili nchini Marekani kupitia Vyuo Vikuu, Radio , mashuleni zikiwemo taasisi
mbalimbali nchini Marekani.

Dkt. Marko J. Mwaipopo kutoka chuo kikuu cha Michigan akielezea uzoefu wa ufundishaji 
wa lugha ya Kiswahili katika vyuo na taasisi nchini Marekani,
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.

Dkt. Mwamoyo Hamza kutoka sauti ya Amerika (VOA) akielezea nafasi ya Kiswahili
katika tasnia ya habari nchini Marekani.

Bi. Jerusha Weaver MPH,CHES kutoka chuo kikuu cha North Carolina mji wa Chapel Hill
akielezea nafasi ya kiswahili katika Diplomasia ya Utamaduni nchini Marekani

Rhonda Pierce mwakilishi wa Tanzania katika taasisi ya Sister City International (SCI)
akielezea nafasi ya Kiswahili katika kuimarisha mahusiano ya miji dada yaArusha, Tanzania na Durham, North Carolina nchini Marekani.

Bi.Jasmine Rubama Mkufunzi wa Kiswahili (Foreign Service Institute) akielezea
mchango wa Diaspora katika kukuza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akitoa
 hotuba ya kufunga maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani na kusisitiza
kwamba ataendelea kuitangaza na kuipigania lugha hiyo na kuhakikisha inafika mbali
 nchini Marekani na kimataifa.

Mshereheshaji Tuma Kaisi akiwajulisha jambo wahudhuriaji kwenye maadhimisho hayo

Juu na chini ni picha za pamoja Waheshimiwa Mabalozi na wadau wa Kiswahili siku ya
maadhimisho hayo Ijumaa July 7, 2023 jijini Washington DC nchini Marekani.
No comments:

Post a Comment