Monday, November 12, 2012

HATIMAYE LIONEL MESSI AVUNJA REKODI YA PELE - AFUNGA MABAO 76 NDANI YA MWAKA


Leo Messi, akiwa na miaka 25 tu, amefikia rekodi ambazo zimefikiwa na magwiji wa soka pekee. Jumapili ya jana, katika dimba la Iberostar, Muargentina huyo aliipita rekodi ya Pele ya kufunga mabao mengi zaidi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Akifunga mbao mawili dhidi ya Mallorca.. Messi sasa amefunga magoli 76 ndani ya mwaka wa 2012. goli moja zaidi ya Pelel aliyefunga mabao 75 katika mwaka 1958.

Magoli 64 kwa Barça, 12 kwa Argentina 

Mabao 48 ya Messi kati ya 76 ndani ya 2012 yalifungwa katika La Liga - 33 katika msimu huu na 15 msimu uliopita. 12 akaifungia Argentina. 

Pelé, kwa upande mwingine alifunga mabao 58 katika mashindano ya Paulista, 8 katika mashindano ya Rio-Sao Paulo, na mabao 9 aliifungia timu yake ya taifa - kati ya mabao yake hayo 9 ya timu ya taifa, sita kati ya hayo yalifungwa katika fainali za kombe la dunia 1958, na mengine aliyafunga katika mechi za kirafiki. 

Málaga and Bayer Leverkusen

Japokuwa Atletico Madrid ndio watu waliojeruhiwa sana Messi, lakini mwaka 2012 timu ambazo zimeonja joto la balaa la Messi ni Malaga na Bayern Leverkusen ambao wote wameambulia kufungwa magoli 6 kila timu.

No comments:

Post a Comment