Monday, January 28, 2013

Didier Drogba ajiunga na Galatasaray

Didier Drogba

Didier Drogba hatimaye amesaini mkataba miezi 18 kuichezea Galatasary baada ya kuipiga chini ofa ya kurudi tena Chelsea. 

Nahodha huyo wa Ivory Coast amejiunga na waturuki kwa mkopo akitokea klabu ya kichina ya Shanghai Shenhua. 

Roman Abramovich alitoa ruhusa wiki iliyopita kutoa ofa ya dili la mkopo mpaka mwishoni mwa msimu, huku kukiwepo na wazo la kumsajili kwa mwaka mwingine zaidi.  

Mazungumzo yalishafikia mbali kiasi na Chelsea wakawa wanaamini kwamba watamsaini tena mwanaume ambaye aliwaletea ubingwa wa kihistoria wa ulaya msimu uliopita kabla ya siku ya mwisho ya usajili alhamisi wiki hii. 

Drogba alishinda makombe matatu ya EPL, manne ya FA, na akamaliza maisha yake ya soka na  Chelsea na ubingwa wa ulaya kwa kuwafunga Bayern  Munich katika fainali. 

Chelsea walimpa ofa ya mwaka mwingine kwenye mkataba wake huku wakipunguza kidogo mapato yake, lakini Drogba aliamua kuondoka na Shanghai Shenhua.

No comments:

Post a Comment