Sunday, March 17, 2013

Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

Absalom Kibanda

TUKIO la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Absalom Kibanda usiku wa kuamkiaJumatano wiki hii, limechukua sura mpya baada ya mtu aliyejitambulisha kama Ridhiwani Kikwete akitumia ukurasa wake wa mtandao wa facebook kutoa maneno ya kejeli, akihoji kama nae ametekwa na Ikulu.

Mbali na Ridhiwani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,naye alitumia mateso ya Kibanda kufanya propaganda chafu, akitoa kauli inayoonesha “anawajua” waliomtesa.

Ridhiwani aliandika: “Je, hii nayo ni kazi ya Rama (Afisa Usalama wa Taifa) wa Ikulu?”

Absalom Kibanda
Rama Ighondu ndiye alitajwa na MwanaHALISI kuhusika na mateso ya Dk. Steven Ulimboka mwaka jana.Kauli hii ilichefua kwa kiwango kikubwa viongozi wa juu wa New Habari, kampuni anayofanyia kazi Kibanda, kiasi cha kumfanya Afisa Mtendaji Mkuu, Hussein Bashe,kuhoji chanzo chake.

Bashe ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, alikwenda mbali zaidi na kuandika maneno makali dhidi yaRidhiwani:“Huwezi kuleta kebehi ya namna hii. Inaonyesha namna gani hufahamu nafasi yako katika jamii.

Funga mdomo kabisa kwa sababu unajaribu kutukana hisia za watu.“Futa kauli yako ya kijinga ya namna hii, hatuwezi kuvumiliakebehi ya kiwango kikubwa namna hii; umelewa madaraka ya kuwa mtoto wa rais, na kudanganywa na hayo mageti ya ikulu, na kudhani unaweza kuleta kebehi na dharau zako katika kila jambo…


“Nakuonya iwe mwanzo na mwisho;usilete kebehi katika jambo hili.Nakuonya,nakuonya, nakuonya usijaribu! Tumekaa kimya…”

Tangu Ighondu alipotajwa na MwanaHALISI kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka, serikali haijamkamata wala kumhoji. Kauli ya jana ya Ridhiwani kuuliza kwa kejeli kama Kibanda naye aliteswa na watu wa Ikulu, imeibua upya hisia mchanganyiko kuhusu sakata hilo, huku watu wengine wakisema mtoto huyo wa rais anamponza baba yake kwa kutokujua wapi atoe kauli gani.

Baadhi ya waliozungumza na gazeti hili wakionesha kukerwa na kauli ya Ridhiwani, walisema mtoto huyo wa rais anafurahia mateso ya wananchi kwa sababu hajui shida zao, na amelewa madaraka yasiyo yake.Wengine wanaojua kuwa Kibanda alimfundisha Ridhiwani alipokuwa anasoma Shule ya Sekondari Shaaban Robert, Dar esSalaam,walisema hii ni dharau na kejeli iliyopitiliza, inayofanana na ukatili.

Mmoja wao alisema kauli ya Ridhiwani inatokana na kujua udhaifu au upendeleo wa serikali,na kwamba baba yake (rais) hawezi kumchukulia hatua. Wapo piawaliofikia mahali wakasema: “Mtoto huyu kuna kitu anakijua…au kuna kitu anajaribu kuficha.” Katika hali isiyokuwa ya kawaida.

Nape naye alitumia ukurasa wa facebook kulijadili suala hili katika muktadha wa kipropaganda, akitaka kuwahusisha watu kadhaa bilakuwataja majina.

Aliandika hivi: “Hili la kutekwa na kupigwa na kuumizwa kiasi hichi (hiki) kaka yangu Kibanda, kila nikilitafakari maneno ya waliosemahakutatawalika na makala za Kibanda mbili au tatu za mwisho kabla ya kuhama chombo cha habari kabla ya anachofanyia kazi sasa vinajirudia kichwani mwangu sana!”

Kauli hii inaakisi maoni kadhaa yanayosambazwa tangu juzi katika maeneo na mitandao kadhaa,yakiwanukuu baadhi ya makada namashabiki wa CCM ambao wanasema wanalenga kuinusuru serikali isihusishwe na tukio la kutekwa kwa Kibanda.

Huku wakijua kuwa Kibanda aliacha kazi Free Media na kuhamia New Habari kwa hiari yake, kama mwajiriwa yeyote, kama alivyowahikuacha kazi New Habari, na Mwananchi kabla hajajiunga na gazeti hili, Nape na wenzake wamediriki kupandikiza propaganda kwamba kuteswa kwake kuna mkono wa mwajiri wake wa zamani.

Gazeti linajua, na Kibanda anajua,kwamba hana uhusiano mbaya na mwajiri wake wa zamani, bali amekuwa akiwindwa na kuandamwana watu wenye mamlaka makubwa sana katika nchi hii kwa muda mrefu kwa sababu za msimamo wake wa kisiasa katika masuala
kadhaa.

Amepata kuitwa na kuonywa mara nyingi dhidi ya msimamo wake katika masuala ya kitaifa, na hasa kwa msimamo wake na makalazinazoonekana wazi kumuunga mkono kigogo mmoja anayechuana na wenzie ndani ya CCM katika kinyang’anyiro cha urais 2015.

Gazeti hili linajua pia kwamba hata mawasiliano ya simu ya Kibanda na baadhi ya wahariri wenzake (na wa gazeti hili wamo) yanafuatiliwa kinyume na sheria.

Kauli yake mwenyewe juzi akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari kabla hajapelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, inadokeza aina ya watuwaliomtesa.

Kibanda alisema kuwa alimsikia mmoja wa watesi wake aliyekuwa na silaha ya moto akikoki risasi na kisha kumuuliza mwenzake, “afande, tummalize?”

Wananchi waliopiga simu chumba cha habari jana baada ya kusoma kauli za Nape na Ridhiwani walisema nukuu hii ya Kibanda ndiyo inawapa kiwewe watu wanaodhani serikali inaweza kuhusishwa na tukio hili dhalimu.

Mmoja wa waliojibu kauli za Nape na Ridhiwani pale pale mtandaoni,aliandika kwa hasira: “Mna dola na all machineries (taasisi zote)mnashindwa nini kuwakamata na kuwachukulia hatua? Lini mtaacha propaganda za kimisukule? “Mwigulu (anadai) anao mkanda,wewe pia unataka kutuaminisha kuwajua wahaini wa Kibanda. Kama kweli acha upuuzi, peleka maelezo polisi. 

Mmeanzisha propaganda za udini, na bado tu hamtuonei huruma tusio na pa kukimbilia?”

Source. Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment