Monday, September 30, 2013

Wengi wamkubali Mh. Mwigulu Nchemba : Hotuba yake yabadili mtazamo wa wengi

Mhe. Mwigulu Nchemba katika picha ya pamoja na Mmsaidizi wa Rais Dkt Jakaya Kikwete
 Mhe. Rajab Luhwavi wakiwa meza kuu kwenye mkutano wa CCM DMV
uliowajumuisha wanaDMV wakiwemo viongozi wa dini na jumuiya ya
Watanzania DMV
.
Baada ya hotuba ya Mhe. Nchemba kilianza kipindi cha maswali na majibu wengi kuonekana kumkubali majibu yake hasa Dotto Mallongo ilipofika zamu yake alikumkubali na kusema "nilikuwa sikufahamu lakini baada ya kukusikiliza nimekuelewa wewe ni kiongozi wa aina gani na nilikua nimekupania sana lakini hotuba yako imenituliza mukali wangu na historia yako ya maisha inafanana na yangu". Kipindi cha maswali na majibu kiliongezwa muda kutokana na waulizaji kuwa wengi na kuonekana kuridhishwa na majibu yaliyojibiwa na Mhe. Nchemba huku akisaidiwa na msaidizi wa Rais Kikwete, Mhe. Rajab Luhwavi.

Maswali yaliyoulizwa ni pamoja na huduma duni za hospitali zetu na kwanini serikali inazidi kujenga hospitali huku hospitali nyingi hazina dawa, na walio wengi wakikerwa na biashara ya madawa ya kulevya jinsi inavyotia fedheha taifa la Tanzania na ni kwanini serikali inasita kuweka majina hazarani huku ikitamka kila siku kwamba inawajua watu wanaouza madawa na majina inayo.

Mhe. Mwigulu Nchemba alijibu maswali hayo kwa kusema ukosefu wa madawa kwenye hospitali zetu ni kutokana na ufinyu wa bajeti lakini serikali inatambua hilo na inalifanyia kazi siku za mbeleni dawa za wagonjwa zitawiyana na hospitali zinazojengwa. Kuhusu kutajwa majina ya wafanya biashara ya madawa ya kulevya Mhe. Nchemba amesema kwa sababu za kiusalama na kwamba swala lipo kwenye vyombo husika na ndio maana majina hayajatajwa kwa kuhofia kuvuruga ushahidi na kuingilia kazi ya vyombo hivyo.

Swali lililowavutia wengi ni pale Ridhiwani Kikwete alipohusishwa na madawa ya kulevywa kwamba alishawahi kukamatwa na madawa nchini China na kutokana na kwamba Ridhiwani ni mtoto wa Rais ndio maana kukatokea makubaliano na China ya kuja Tanzania na kusaini mikataba 18 isiyokuwa wazi.

Mhe. Mwigulu Nchemba alisema habari hiyo ya Ridhiwani sio ya kweli na akatoa mfano alipokuja Rais Baraka Obama wakati wa maswali ya waandishi habari liliulizwa swala kuhusu Afisa wa Ubalozi aliyehusishwa na kumnyanyasa mfanyakazi wake je kama Ridhiwani Kikwete anajihusisha na madawa ya kulevya wangeshindwaje kuuliza swala hilo na unavyojua Wamarekani hawamuonei mtu aibu, Je inakuingia akilini kweli eti Ridhiwani abebe madawa yeye mwenyewe? aliendelea kwa kusema haya ni maneno ya kutengeneza tu hayana ukweli wowote. Hotuba nzima na maswali na majibu tutawaletea baadae.

Picha ya pamoja meza kuu
Msaidizi wa Rais Kikwete Mhe. Rajab Luhwavi akijibu baadhi ya
maswali yaliyokuwa yakiulizwa kwenye mkutano wa CCM
uliowajumuisha wa Tanzania DMV.
Afisa Mindi Kasiga akifuatilia mkutano kulia ni mama Winy Casey
Viongozi wa CCM - North Carolina kushoto ni David Mushi, Mwenyekiti wa Tawi na
Festo Mombo Katibu wa Tawi.
Juu na chini wanaCCM na Watanzania DMV wakifuatilia mkutano
kwa picha zaidi bofya read more.

Mselemu katika picha.
Mwenyekiti CCM DMV akifunga mkutano
Picha ya pamoja.
































No comments:

Post a Comment