Monday, November 18, 2013

Msiba Houston , Texas na Dar es Salaam

Marehemu Bibi Hawa Kamanga 1941-2013
Wanajumuiya wenzetu Haji, Kaela, na Hizza Kamanga wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Mrs Hawa Haji Kamanga  kilichotokea Dar es salaam siku ya Jumatatu tarehe 18 Nov 2013.Mama Hawa Kamanga ambaye alifariki leo hii asubuhi mnamo saa 2:40 katika hospitali maalum ya wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam ameacha watoto 6, wa kiume watano na wa kike mmoja. Kati ya hao watatu wanaishi marekani nao ni Haji, Kaela na Hizza.Wengine wawili wa kiume wanaishi Tanzania ambao ni  Zakaria (kaka mkubwa) na Pioka. Na mmoja wa kike Anna Kange anaishi Holland, Marehemu ameacha wajukuu 11 na kitukuu mmoja. 

Baada ya wanafamilia kukaa kikao, imeamuliwa kuwa marehemu atazikwa kesho saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu na shughuli zote za msiba zipo Sinza Vatican. 

Kwa Houston , Texas wafiwa wanapatika kwenye anwani hii :

7107 Crim Lilly Ct  , Cypress TX 77433

Namba ya Haji 281 236 8379
Namba ya Hizza 281 865 3709
Namba ya Kaela 713 884 7950

MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI! AMIN

Chanzo cha habari na picha Hizza Kamanga,Grace Mmari, Houston Texas / Tausi Khalid Dar, Tanzania.

No comments:

Post a Comment