Monday, November 18, 2013

Picha za Kisomo nyumbani kwa Mahundi Family, Brooklyn New York

Maustadh wakisoma dua katika kisomo hicho cha kumuombea marehemu Bi Mwanakondo Jumbe Mmanga mama yake na Latifa, kifo hicho kimetokea Tanzania siku ya Jumapili alfajiri na kuzikwa jioni ya jumapili hiyo hiyo huko Tanzania. Watanzania wa New York na sehemu za jirani walikusanyika nyumbani kwa wafiwa familia ya Mahundi kutoa pole na kushiriki kisoma cha kumuombea marehemu.
Watanzania wakiwa nyumbani kwa Latifa na wadogo zake huko Brooklyn NY, nyumba ilikuwa imefurika Watanzania hii ni kuonyesha upendo kwa familia ya Mahundi hasa kwa kipindi hiki kigumu kwao kutokana na kifo kilicho wakuta. Familia ya Mahundi yenye watoto wakike wa 3 Latifa, Hamisa, na Bahia na pia kuna kaka yao anaeitwa Ashraf. Familia hii siku zote hipo msitari wa mbele kwenye shughuri zozote zinazo husu Watanzania  ndiyo maana watu walivyosikia juu ya msiba walijitokeza kwa wingi nyumbani kwa wafiwa ili kujumuika nao katika kipindi hiki kigumu kwao kwa kuondokewa na mzazi huyo wa Latifa na ni bibi wa akina Hamisa, Bahia na Ashraf.
Hapa mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania wa New York bwana Hajji Khamis akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Springfield MA bwana Isaac Kibodya alikuwepo nae nyumbani kwa wafiwa hapa akiongea machache.
Mwanamusiki anayefanya vizuri kwenye anga ya muziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania Mwana FA alipata fursa ya kupia msibani hapo kuwafariji wafiwa.
Bwana Bilal fundi mzuri sana wa kupika biriyan ukiwa na shughuri za msiba na harusi akipata ukodak na Mwanafa. Kwaiyo ukiwa na Harusi au sherehe yeyote Bilal ndiyo suluhisho lako.

Kutoka kushoto ni Mwana FA, Dj Rich Maka na Mkuu wa Wilaya Springfield, MA Bwn. Isaac Kibodya.

Mashabiki wa Mwana FA wakipata Ukodak Moment na mwanamuziki huyo
 Kwa picha zaidi bonyeza soma zaidi.
Watazanzania wakiwa nyumbani kwa wafiwa wakati kisomo kikiendelea
Mweka hazina wa New York Community bwana Faida(wapili toka kulia) alikuwepo nae.
Watanzania wakisoma dua

No comments:

Post a Comment