Friday, April 29, 2016

Watanzania waishio Houston , Texas wachangia ujenzi Matundu 8 ya choo shule ya msingi Nyamajashi

Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston jimboni Texas , Marekani wameonyesha mfano wa kuigwa kwa jumuiya za Watanzania wanaoishi kwenye DIASPORA kwa kuchangia ujenzi wa choo cha matundu 8 ya kisasa kinachotumia maji chenye thamani ya Tshs.7,589,500/= ( Wana Houston wakichangia Tshs.3,200,000/=) katika shule ya msingi Nyamajashi iliyoko kata ya Lamadi wilaya ya Busega,  mkoani Simiyu.

Diwani wa Kata ya Lamadi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Joseph Goryo "Kada" aliomba msaada huo kwa wana-Houston baada ya kuona hali mbaya shuleni hapo ambapo jumla ya wanafunzi 1529 walikuwa wanajisaidia vichakani baada ya kukosekana huduma ya choo. 

Uzinduzi wa choo hicho kipya ulifanywa na mkuu wa Wilaya ya Busega Bw.Paul Mzindakaya

Diwani wa Lamadi Bw. Joseph Goryo kwenye uzinduzi 
Jiwe la msingi linavyosomeka siku ya ufunguzi
Diwani akikabidhiwa Shahada ya kutambua mchango wake kwenye ujenzi
Mwalimu mkuu Bw. Karol Cleophace Wanjara akiwa na Diwani Goryo 


No comments:

Post a Comment