Sunday, November 28, 2021

SIMBA (UGHAIBUNI) YAICHAPA YANGA (UGHAIBUNI) 4-2

Timu ya Simba (Ughaibuni) usiku wa jana iliichabanga bila huruma Yanga (Ughaibuni) jumla ya mabao 4-2 katika mechi kali ya iliyofanyika katika viwanja vya Cullen Park jijini Houston, Texas. Wakiongozwa na kiungo mkongwe Rahim Chomba Veron iliwachukua Simba dakika 25 kuandika bao la kwanza kupitia kwa striker machachari Mark Maonyesho aka Sancho. Simba iliandika bao la pili dakika ya 32 kupitia kwa Peter Dotto baada ya kugongeana pasi zaidi ya 6 na wachezaji wenzake. Simba iliendelea kulisakama lango la Yanga kama nyuki na kujipatia bao la 3 katika dakika ya 41 kipindi cha kwanza kupitia kwa Mark Maonyesho tena aliyemalizia pasi nzuri ya Adrian Muhabuki. 

Yanga ilizinguka na kupeleka mashambulizi makali langoni mwa Simba na kujipatia bao la kwanza katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa Eric Sabith Mayele baada ya kugongewa pasi safi na kiungo Maneno Ngolo Makambo. Hadi mapumziko Simba ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili Simba iliendelea kutawala mchezo na kujipatia bao la nne katika dakika ya 65 kupitia kwa MZ aliyemalizia kazi nzuri ya Mudhihir Said aka Nungunungu. Yanga walipata bao la 2 dakika za mwishoni za mchezo baada ya Ally Abaenya kumalizia pasi ya mkongwe Ally Ndikumana maarufu kama Ntibanzokinza.































































































































































No comments:

Post a Comment